Jumatatu 20 Aprili 2026 - 00:19
Radi amali ya Ayatullah Jawadi Amoli kuhusu kumdhalilisha Papa/ Heshima ya viongozi wa kidini duniani lazima ihifadhiwe

Hawza/ Mtukufu Ayatullah Jawadi Amoli katika ujumbe wake alielezea masikitiko yake juu ya dharau iliyofanywa na Rais wa Marekani dhidi ya Papa Leo wa Kumi na Nne, kiongozi mkuu wa Wakatoliki duniani, na akasisitiza juu ya ulazima wa jamii ya Wakristo na shakhsia za kidini duniani kukosoa na kupinga vikali dhidi ya mwenendo huu.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, Mtukufu Ayatullah Jawadi Amoli katika ujumbe wake alielezea masikitiko yake juu ya dharau iliyofanywa na Rais wa Marekani dhidi ya Papa Leo wa Kumi na Nne, kiongozi mkuu wa Wakatoliki duniani, na akasisitiza juu ya ulazima wa jamii ya Wakristo na shakhsia za kidini duniani kukosoa na kupinga vikali dhidi ya mwenendo huu, na akasema: dharau iliyofanywa dhidi ya hadhi tukufu ya kiongozi wa Wakatoliki duniani lazima ifidiwe na kurekebishwa.

Ayatullah Jawadi Amoli katika ujumbe wake, huku akibainisha kwamba Mtukufu Nabii Issa Masihi (sa) ni miongoni mwa Mitume wa Ulul-Azm na ni ishara ya Mwenyezi Mungu, alisema: Qur’ani Tukufu humtaja Masihi (sa) na mama yake Maryam kwa utukufu na adhama; Mtukufu Issa na mama yake Maryam (as) ni ishara ya ulimwengu mzima, na ni wenye kuheshimiwa na kuthaminiwa kwa wanadamu wote, na kuwaheshimu, kuwatazimia na kuwapa heshima hawa watakatifu ni wajibu juu ya watu wote.

Mtukufu huyo alisema: ikiwa Qur’ani kuhusu Nabii Nuhu inasema: {سَلَامٌ عَلَی نُوحٍ فِی الْعَالَمِینَ} na ikiwa kuhusu Mtume inasema: {رَحْمَةً لِلْعَالَمِینَ}, na ikiwa kuhusu Maryam na mwanawe Issa ina ibara zinazofanana na hizi, basi maana yake ni kwamba jukumu la walimwengu ni kunyenyekea mbele ya watakatifu hawa, kuihifadhi heshima yao, na ikiwa mtu alikuwa kiongozi wa kidini wa Mitume kama hawa, basi naye pia anaheshimiwa na ana heshima maalumu na ya kipekee; si wafuasi wa Mtukufu Issa tu, bali pia wafuasi wa dini nyingine na Mitume wengine wanapaswa kuhifadhi heshima yao.

Mtukufu Ayatullah Jawadi Amoli alisema: Qur’ani Tukufu imetaja mafundisho ya Issa Masihi kuwa ni hekima: {قَدْ جِئْتُکُمْ بِالْحِکْمَةِ}; maana ya hekima ni kwamba jamii ya wanazuoni, yaani hawza za kielimu, vyuo vikuu, na vituo vya fikra na utamaduni, katika upande wa fikra wawe na fikra zilizo safi, sahihi na zenye uhalisia, na katika upande wa motisha wawe na motisha ya kiakili, sahihi na yenye manufaa mema.

Mtukufu huyo aliendelea kusema: kwa masikitiko, Rais wa Marekani ambaye hana usahihi katika fikra wala katika motisha, na hakuna usahihi wala manufaa katika kazi zake za kielimu wala za kiutendaji, kwa ujasiri amefanya dharau na utovu wa adabu dhidi ya heshima takatifu ya hadhi tukufu ya kiongozi wa Wakatoliki duniani; Wakristo kwa ujumla, na Wakatoliki pamoja na wakubwa waliomo ndani ya Marekani hasa, wanapaswa kuukataza uovu huu na kulaani ubaya huu, na wamfundishe na kumlea mwenye kauli hii, japokuwa yeye si mwenye kukubali kulelewa.

Aliongeza kuwa: Rais wa Marekani kwa kushirikiana na Israel wamefanya dhulma iliyo wazi na kubwa dhidi ya Iran ambayo ina historia ndefu katika utamaduni, dini na malezi; hawa si kwamba wamewashambulia watu wa kijeshi pekee, bali pia wasiokuwa wa kijeshi, wanawake, wasomi, wasanii, watoto na wadogo, wasichana na wavulana wa shule ya Minab ambao walikuwa mfano wa kudhulumiwa; wamewaua wengi wa wapendwa hawa na kuwafanya waliobaki kuwa na huzuni na majonzi; kila msiba wa namna hii ni wa kuumiza moyo na wa kusikitisha; na mbele ya jinai za aina hii ambazo Trump na mfano wake wamefanya, ushauri wa kiongozi wa Wakatoliki duniani dhidi ya dhulma hii ya wazi ni kauli yenye thamani kubwa, na haipaswi mtu yeyote kupinga mbele ya nasaha na uongozi huu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha